البقرة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَٱتَّقُوا۟ يَوْمًا لَّا تَجْزِى نَفْسٌ عَن نَّفْسٍ شَيْـًٔا وَلَا يُقْبَلُ مِنْهَا شَفَـٰعَةٌ وَلَا يُؤْخَذُ مِنْهَا عَدْلٌ وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ ٤٨
(48) Na akawahofisha na Siku ya Kiyama ambayo, "hatomfaa mtu" hata ikiwa ni katika nafsi tukufu zaidi kama vile Manabii na watu wema. "Mtu" hata kama ni wa ukoo wa karibu zaidi "chochote" siyo kikubwa wala kidogo. Lakini binadamu yatamnufaisha tu matendo yake ambayo alitanguliza mbele. "Wala hayatakubaliwa kwake maombezi" kwa yeyote bila ya idhini ya Mwenyezi Mungu na kumridhia kwake yule anayeombewa. Na wala haridhii katika matendo isipokuwa yale yaliyokusudiwa kwayo uso wake, na yalikuwa kwenye Njia na Sunnah. "Na wala hakitapokewa kikomboleo kutoka kwake" na lau kuwa kila nafsi iliyodhulumu inamiliki kila kilimo katika ardhi pamoja na mfano wake; bila shaka ingelitoa fidia vyote kujikomboa kutokana na adhabu ya Mwenyezi Mungu, na wala halitakubaliwa hilo kutoka kwao. "Wala hawatanusuriwa" yani hawataondolewa machukizo hayo. Basi akakanusha kunufaika kutoka kwa viumbe kwa namna yoyote ile. Hivyo, kauli yake "mtu hatomfaa mtu kwa chochote,” ni katika kutafuta manufaa, "wala hawatanusuriwa" hili ni katika kuzuia madhara. Na huku ni kukanusha jambo ambalo mwenye kunufaisha anajiwa nalo. "Wala hayatakubaliwa kwake maombezi, wala hakitapokewa kikomboleo kwake." Na huku ni kukanusha (kupata) manufaa yanayoombwa kutoka kwa anayeyamiliki kwa kubadilishana, kama vile uadilifu, au kwa kitu kingine, kama vile uombezi. Kwa hivyo, hili linamlazimu mja kuukata moyo wake kutokana na kufungamana na viumbe akishajua kuwa wao hawatamanufaisha uzito wa chembe, na kwamba aufungamanishe na Mwenyezi Mungu ambaye analeta manufaa, na anazuia madhara. Basi amuabudu Yeye peke yake, hana mshirika yeyote, na amtake msaada katika kumuabudu.