البقرة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ وَكَذَّبُوا۟ بِـَٔايَـٰتِنَآ أُو۟لَـٰٓئِكَ أَصْحَـٰبُ ٱلنَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَـٰلِدُونَ ٣٩
(39) Na vile vile, kukanusha upotovu na uovu juu ya mwenye kufuata uwongofu wake. Na viwili hivi visipokuwepo, basi kinyume chake kinathibiti, nao ni uwongofu na kufaulu. Hivyo basi, mwenye kufuata uwongofu wake, atapata amani na kufaulu duniani na akhera, na uwongofu, na akaepuka kila yanayochukiza kama hofu, huzuni, upotovu, uovu, basi akapata kinachopendeza, na akaepuka kinachohofiwa. Na huyu ni kinyume cha mwenye kutofuata uongofu wake, akaukufuru na akakadhibisha aya zake. Basi hao ndio watakaokuwa wenza wa Moto. Yani watakaokaa pamoja nao kama vile mwenza anavyokaa pamoja na mwenza wake, na mdaiwa na mdai wake “humo watadumu.” Hawatatoka nje yake wala adhabu haitawaisha, na wala hawatasaidiwa. Na katika aya hizi na mfano wake, kuna kugawanyika kwa viumbe: Majini na wanadamu katika wale kufaulu na wale wa kuhasiri. Na ndani yake kuna sifa za makundi haya mawili na matendo yanayosababisha hayo. Na kwamba majini ni kama wanadamu katika malipo na adhabu, kama walivyo sawa katika amri na makatazo.