انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · البقرة
السورة ٢

البقرة

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٢٧٦

يَمْحَقُ ٱللَّهُ ٱلرِّبَوٰا۟ وَيُرْبِى ٱلصَّدَقَـٰتِ ۗ وَٱللَّهُ لَا يُحِبُّ كُلَّ كَفَّارٍ أَثِيمٍ ٢٧٦

{276} Kisha Mwenyezi Mungu akajulisha kwamba Yeye huyaondolea baraka mapato ya wenye riba, na huzibariki sadaka za wenye kutoa. Kinyume na inavyotangulia kuwajia wengi wa viumbe kwamba kutoa matumizi kunapunguza mali, na kwamba riba inaizidisha. Lakini asili ya riziki na kupata matunda yake ni kutoka kwa Mola Mtukufu. Na kile kilicho kwa Mwenyezi Mungu hakipatikani isipokuwa kwa kumtii Yeye na kufuata amri yake. Kwa hivyo mwenye kujasiri kuingia katika riba, ataadhibiwa kwa kinyume cha makusudio yake. Na hili linashuhudiwa kwa tajiriba. Na ni nani mkweli zaidi kwa usemi kuliko Mwenyezi Mungu. "Na Mwenyezi Mungu hampendi kila mwenye kukufuru, afanyae dhambi." Naye ni yule aliyekufuru neema ya Mwenyezi Mungu, na akaikanusha hisani ya Mola wake Mlezi, na akapata dhambi kwa kuendelea kwake kumuasi. Maana isiyokuwa ya moja kwa moja ya Aya hii ni kwamba Mwenyezi Mungu humpenda kila mwenye kushukuru kwa neema, mwenye kutubia maovu na dhambi. Kisha akaiingiza Aya hii kati ya Aya za riba, nayo ni kauli yake: