انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · البقرة
السورة ٢

البقرة

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٢٧٣

لِلْفُقَرَآءِ ٱلَّذِينَ أُحْصِرُوا۟ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ لَا يَسْتَطِيعُونَ ضَرْبًا فِى ٱلْأَرْضِ يَحْسَبُهُمُ ٱلْجَاهِلُ أَغْنِيَآءَ مِنَ ٱلتَّعَفُّفِ تَعْرِفُهُم بِسِيمَـٰهُمْ لَا يَسْـَٔلُونَ ٱلنَّاسَ إِلْحَافًا ۗ وَمَا تُنفِقُوا۟ مِنْ خَيْرٍ فَإِنَّ ٱللَّهَ بِهِۦ عَلِيمٌ ٢٧٣

{273} Anamaanisha kwamba, mfanye hima kuwajua mafakiri ili muwape sadaka zenu ambao walijizuilia nafsi zao katika njia ya Mwenyezi Mungu na utiifu wake. Na hawana nia ya kuchuma (kutoka kwa sadaka) wala hawana uwezo wa kuchuma. Nao wanajizuia kiwango kwamba wasiowajua wakiwaona, wanafikiri kwamba wao ni matajiri. "Hawawang'ang'anilii watu kwa kuwaomba." Wao hawaombi kabisa, na hata wakiomba kwa sababu ya dharura hawang'ang'anilii katika kuomba. Na aina hii ya mafakiri ndiyo bora zaidi ya kuyaweka matumizi haya ndani yao ili kuzuia mahitaji yao na kuwasaidia katika makusudio yao. Na njia ya heri na kuwashukuru juu ya kile wanachosifika kwacho cha subira, na kumtazama Muumba na siyo viumbe. Na pamoja na hayo, kutoa kutumia katika njia za wema, na juu ya wenye mahitaji popote pale walipo, ni jambo la heri na lenye malipo na thawabu kwa Mwenyezi Mungu. Na kwa sababu ya hili akasema: