البقرة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
قَوْلٌ مَّعْرُوفٌ وَمَغْفِرَةٌ خَيْرٌ مِّن صَدَقَةٍ يَتْبَعُهَآ أَذًى ۗ وَٱللَّهُ غَنِىٌّ حَلِيمٌ ٢٦٣
{263} Mwenyezi Mungu alitaja daraja nne za ihsaan: Daraja la juu zaidi: Kutoa kunakotokana na nia njema, na aliyetoa hakukufuatisha masimbulizi wala maudhi. Kisha linafuatwa na kusema mema. Nalo ni kufanya ihsani katika kuzungumza kwa aina zake zote, ambako ndani yake kuna kumfurahisha Muislamu. Na kutaka udhuru kutoka kwa mwombaji ikiwa hatapata kitu kutoka kwake, na yasiyokuwa hayo katika maneno mema. Na la tatu ni kufanya ihsani kwa kumsamehe na kutupilia mbali aliyekufanyia ubaya kwa kauli au kitendo. Na mawili haya ni bora kuliko la nne na la heri zaidi kuziliko. Nalo ni lile ambalo mwenye kutoa sadaka anafuatisha maudhi kwa aliyempa. Kwa sababu aliharibu wema wake na akafanya mema na mabaya. Basi heri tupu, hata kama ni chache, ni bora kuliko heri iliyochanganyika na shari hata kama ni nyingi. Na katika hili, kuna tahadharisho kubwa kwa anayemuudhi yule anayempa sadaka, kama wanavyofanya watu wachoyo, wapumbavu na wajinga. "Na Mwenyezi Mungu" Mtukufu "ndiye Mwenye kujitosheleza" kwa kutohitaji sadaka zao. Na pia hawahitaji waja wake wote "Mpole" pamoja na ukamilifu wa kujitosheleza kwake, na wasaa (wingi) wa vipawa vyake. Anawafanyia upole waasi, na wala hawaharakishii kuwaadhibu. Bali huwaweka salama, na kuwaruzuku, na kuwapa heri zake nyingi, na huku wao wanamkabili kwa maasia. Kisha akakataza vikali masimbulizi na maudhi, akayapigia mfano hayo: