البقرة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
يَسْـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلشَّهْرِ ٱلْحَرَامِ قِتَالٍ فِيهِ ۖ قُلْ قِتَالٌ فِيهِ كَبِيرٌ ۖ وَصَدٌّ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ وَكُفْرٌۢ بِهِۦ وَٱلْمَسْجِدِ ٱلْحَرَامِ وَإِخْرَاجُ أَهْلِهِۦ مِنْهُ أَكْبَرُ عِندَ ٱللَّهِ ۚ وَٱلْفِتْنَةُ أَكْبَرُ مِنَ ٱلْقَتْلِ ۗ وَلَا يَزَالُونَ يُقَـٰتِلُونَكُمْ حَتَّىٰ يَرُدُّوكُمْ عَن دِينِكُمْ إِنِ ٱسْتَطَـٰعُوا۟ ۚ وَمَن يَرْتَدِدْ مِنكُمْ عَن دِينِهِۦ فَيَمُتْ وَهُوَ كَافِرٌ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ حَبِطَتْ أَعْمَـٰلُهُمْ فِى ٱلدُّنْيَا وَٱلْـَٔاخِرَةِ ۖ وَأُو۟لَـٰٓئِكَ أَصْحَـٰبُ ٱلنَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَـٰلِدُونَ ٢١٧
Na kwa vile amri ya kupigana vita lau kuwa haikuwekwa katika wakati maalumu, basi ingejumuisha miezi mitukufu na mingineyo, Mwenyezi Mungu akaondoa kupigana vita katika miezi mitukufu, akasema:
(217) Wengi wa wanachuoni wanaona kuwa uharamu wa kupigana vita katika miezi mitukufu ulibatilishwa kwa amri ya kupigana vita na washirikina popote wanapopatwa. Na baadhi ya wafasiri walisema: Haikubatilishwa. Kwa sababu Al-Mutlaq (andiko ambalo halikufungiwa) linapaswa kueleweka kwa mujibu wa Al-Muqayyad (andiko lililofungiwa). Na Aya hii inafunga ujumla wa amri ya kupigana bila mipaka. Na kwa sababu miongoni mwa sifa maalumu za miezi mitukufu, bali sifa kubwa mno yake ni kuharamisha kupigana vita ndani yake. Na hilo linakuwa tu katika kuanzisha kupigana vita. Ama kupigana vita kwa sababu ya kujikinga, huko kunaruhusika katika miezi mitukufu, kama vile kunavyoruhusika katika nchi tukufu. Na kwa kuwa Aya hii iliteremka kwa sababu ya yale yaliyotokea kwa kikosi cha kijeshi cha ‘Abdullah bin Jahsh, na kumuua kwao ‘Amr bin Al-Hadhrami, na kuchukua kwao mali zao, na hilo lilikuwa - kulingana na ilivyosemwa - katika mwezi wa Rajab. Washirikina wakawakosoa kwa kupigana vita katika miezi mitukufu. Nao walidhulumu katika kuwakosoa kwao. Kwani, walikuwa na baadhi ya mabaya ambayo baadhi yake yalikuwa makubwa zaidi kuliko yale waliyowakosoa kwayo Waislamu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kueleza yaliyomo ndani yao, "na kuzuia kuiendea Njia ya Mwenyezi Mungu." Yani washirikina kumzuia anayetaka kumwamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na kumtesa aliyemwamini, na juhudi zao za kuwageuza waiache dini yao. Na ukafiri wao unaotokea katika mwezi mtukufu na nchi takatifu ambao wenyewe tu unatosha kuwa shari kubwa mno. Basi itakuwaje na yalikuwa hayo katika mwezi mtakatifu na nchi takatifu? “Na kuwatoa watu wake.” Yani watu wa Msikiti Mtakatifu, ambao ni Nabii rehema na amani za, swala na salamu za Mwenyezi Mungu Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, na maswahaba wake. Kwa sababu wao ndio wanaoustahiki zaidi kuliko washirikina. Nao ndio wanauimarisha kwa uhakika, basi wakatoa “humo” Na hawakuwawezesha kuufikia, pamoja na kwamba nyumba hii ni sawasawa kwa anayekaa ndani yake na wageni. Na mambo haya kila moja kati yake ni “jambo kubwa zaidi kuliko kuua,” katika mwezi mtukufu. Basi vipi na ilhali yote yamekujumuika ndani yao? Kwa hivyo, ikajulikana kwamba wao ni wapitao mipaka, madhalimu katika kuwakemea kwao Waumini. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akajulisha kuwa kamwe hawataacha kupigana vita na Waumini, na lengo lao si katika mali yao na kuwaua, bali lengo lao ni kuwarudisha kutoka katika Dini yao, na wawe makafiri baada ya Imani yao ili wawe miongoni mwa wenza Moto mkali. Kwa hivyo, wanatoa uwezo wao katika hilo, kwa kujitahidi namna wawezavyo. “Lakini Mwenyezi Mungu amekataa isipokuwa kutimiza nuru yake, hata kama makafiri watachukia.” Na sifa hii ni ya jumla kwa makafiri wote. Wao hawaachi kuwapiga vita wasiokuwa wao mpaka wawarudishe kutoka katika dini yao. Hususan Watu wa Kitabu kama vile Mayahudi na Wakristo, ambao walifanya juhudi za kuanzisha taasisi mbalimbali, na wakaeneza walinganizi, na wakaeneza madaktari, na wakajenga shule, ili kuwavutia mataifa kwenye dini yao. Na kuingiza ndani yao kila wawezalo katika fikira potofu ambazo zinawafanya kuwa na shaka juu ya dini yao. Lakini linalotarajiwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu aliyewaneemesha Waumini kwa Uislamu, na akawachagulia Dini yake iliyonyooka sawa. Na akawakamilishia Dini yake ni kwamba atawatimizia neema yake waweze kuisimamia kusimama kukamilifu. Na kwamba asimsaidie kila anayetaka kuizima nuru yake, na atie vitimbi vyao kwenye shingo zao, na ainurusu Dini yake; na aliinue juu neno lake. Na Aya hii inakuwa kweli kwa hawa walio miongoni mwa makafiri, kama ilivyokuwa ya kweli juu ya wale waliokuwa kabla yao. “Hakika, wale waliokufuru hutoa mali zao ili kuzuia Njia ya Mwenyezi Mungu. Basi watazitoa, kisha zitakuwa majuto juu yao, na kisha watashindwa. Na wale waliokufuru watakusanywa kwenye Jahannam.” Kisha Mola Mtukufu akajulisha kwamba mwenye kuacha Uislamu kwa kuuchagua ukafiri badala yake. Na akaendelea na hilo mpaka akafa hali ya kuwa ni kafiri; “basi hao ndio ambao matendo yao yameharibika katika dunia na Akhera.” Kwa sababu kukosekana kwa sharti lake, ambalo ni Uislamu. “Na hao ndio wenza wa Moto. Wao humo watadumu”. Na Aya hii iliashiria kwa maana yake isiyo ya moja kwa moja kuwa, mwenye kuritadi kisha akarejea katika Uislamu, yanamrudia matendo yake yaliyokuwa kabla ya kuritadi kwake. Na vile vile mwenye kutubu akaacha dhambi, basi yeye pia matendo yake yaliyotangulia yatarudia.