انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · البقرة
السورة ٢

البقرة

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٧٩

وَلَكُمْ فِى ٱلْقِصَاصِ حَيَوٰةٌ يَـٰٓأُو۟لِى ٱلْأَلْبَـٰبِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ١٧٩

Kisha Mola Mtukufu akabainisha hekima yake kubwa katika kuweka sheria ya kulipiza kisasi, akasema:

“Mtakuwa nao uhai mzuri katika kulipiza kisasi” yani damu zitahifadhika kwa hilo, na watazuilika waovu kwa hilo. Kwa sababu anayejua kwamba yeye atauawa akiua, basi haitakaribia kuua kutokea kwake. Na muuaji anapoonekana ameuawa, basi asiyekuwa yeye ataogopa na kukomeka. Na lau kuwa adhabu ya muuaji haingekuwa siyo kuua, basi haingezuilika shari (uovu) kama kule kuzuilika kunakotokana (kutekeleza adhabu ya) na kuua. Na vivyo hivyo adhabu za kisheria zote zenye kinaya na kukomeka kuna kile kinachoonyesha hekima ya Mwenye hekima, Mwenye kusamehe. Na neno “uhai” limeachwa katika hali ya nomino ya kawaida ili iwe na maana ya utukufu na wingi. Na kwa vile hukumu hii haijui uhalisia wake isipokuwa wenye akili timilifu na wenye ufahamu mkubwa, amewahusisha na usemi huu na siyo wasiokuwa wao. Na hili linaashiria kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu anapenda kwa waja wake kwamba, wazitumie fikira zao na akili zao katika kutafakari zile hekima zilizoko katika hukumu zake na masilahi yanayoashiria ukamilifu wake, na ukamilifu wa hekima yake, na sifa zake na uadilifu, wake na rehema yake pana. Na kwamba yeyote aliye katika daraja hii, basi anastahiki kusifiwa katika wenye akili ambao usemi huu ulielekezwa kwao, na akawaita Mola Mlezi wa mabwana wote. Na hiyo inatosha kuwa fadhila na heshima kwa watu wanaotumia akili zao. Na kauli yake, “ili mpate kuwa wachamungu.” Na hilo ni kwamba anayemjua Mola wake Mlezi na anayajua yaliyomo katika dini yake, na sheria miongoni mwa siri kubwa na hekima ya ajabu na Aya (ishara) tukufu. Hayo yatamlazimu kufuata amri ya Mwenyezi Mungu, na kuyaona maasia yake kuwa jambo kubwa, ili ayaache. Kwa hivyo akastahiki kwa hayo kuwa miongoni mwa wachamungu.