البقرة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَمَثَلُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ كَمَثَلِ ٱلَّذِى يَنْعِقُ بِمَا لَا يَسْمَعُ إِلَّا دُعَآءً وَنِدَآءً ۚ صُمٌّۢ بُكْمٌ عُمْىٌ فَهُمْ لَا يَعْقِلُونَ ١٧١
Mwenyezi Mungu Mtukufu alipobainisha kutofuata kwao yale waliyoyaleta Mitume, na kukataa kwao hayo kwa kuwaiga baba zao; ikajulikana kwa hilo kwamba wao hawataikubali haki, wala hawatamuitikia. Bali ilikuwa ishajulikana kwa kila mtu kwamba hawataacha kuendelea na ukaidi wao. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu Mtukufu akapeana habari kwamba mfano wao anapowalingania mlinganiaji kwenye imani, ni kama mfano wa wanyama ambao mchungaji wao huwaongelesha kwa sauti kubwa. Ilhali wao hawafahamu kile anachokisema mchungaji huyo wao na mwitaji wao. Wao (washirikina) wanasikia sauti tu, ambayo kwayo hoja inasimama juu yao, lakini hawaielewi kuelewa kwa kuwanufaisha. Ndio maana, wakawa viziwi wasioisikia haki; kusikia kwa kuelewa na kuikubali. Vipofu wasioona kuona kwa kuzingatia, mabubu wasioweza kutamka yale yenye kheri kwao. Na sababu yenye kuleta haya yote ni kwamba hawana akili timamu, bali wao ndio wajinga wa wajinga wote, na wapumbavu wa wapumbavu wote. Basi je, mwenye akili timamu anaweza kuwa na shaka kuwa mwenye kuitwa kwenye uwongofu, na akatenganishwa na ufisadi, na akakatazwa kuingia ndani ya adhabu? Na akaamrishwa yale yenye kutengenea kwake, kufaulu kwake, mafanikio yake, na neema yake, kisha akamuasi huyo mwenye kumshauri na akajitenga na amri ya Mola wake Mlezi? Na akaingia Motoni kwa kujua, na akafuata batili (uongo), na akatupa haki, - ya kuwa huyu hana akili yoyote? - Na kwamba ikiwa pia anasifika kwa hila, na hadaa, na ujanja, basi huyo ndiye mjinga wa wajinga wote.