انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · البقرة
السورة ٢

البقرة

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٦٨

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ كُلُوا۟ مِمَّا فِى ٱلْأَرْضِ حَلَـٰلًا طَيِّبًا وَلَا تَتَّبِعُوا۟ خُطُوَٰتِ ٱلشَّيْطَـٰنِ ۚ إِنَّهُۥ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ ١٦٨

(168) Haya ni maneno kwa watu wote, Waumini wao na makafiri wao. Basi akawaonyesha ihisani kwamba aliwaamrisha wale kila kilichomo ardhini, kama nafaka, mazao, matunda na wanyama hali ya kuwa ni “halali.” Yani kwa namna inaruhusika kwenu kuvitumia, sio kwa nguvu wala kwa wizi, wala kuvipata kwa mapatano ya haramu au kwa namna iliyo haramu; au kwa kusaidia juu ya kilicho haramu. “Na vizuri,” yani sio vibaya kama vile nyamafu, damu, nyama ya nguruwe na machafu yote. Na katika Aya hii, kuna dalili ya kwamba hali ya asili katika vitu ni kuruhusiwa: Kula na kunufaika. Na kwamba kilichoharamishwa ni aina mbili: Ima kimeharamishwa chenyewe, nacho ndicho kichafu ambacho ni kinyume cha kizuri. Na ima ni haramu kwa sababu ya kilichokifikia, hivyo ni haramu kwa sababu kinaambatana na haki ya Mwenyezi Mungu, au haki ya waja wake, na hiki ni kinyume cha halali. Na kuna dalili ya kwamba ni lazima kula kadri inavyoweka muundo sawa. Na mwenye kuacha anapata dhambi kwa sababu ya inavyoonekana katika udhahiri wa amri hii. Na alipowaamrisha kuyafuata yale aliyowaamrisha, - kwa kuwa huko ndiko kutengea kwao kwenyewe, - akawakataza kufuata “nyayo za Shet'ani.” Yani njia zake ambazo yeye huziamrisha. Nazo ni madhambi yote kama vile kufuru, kupindukia mipaka, dhuluma, na inaingia ndani ya hilo kuharamisha Assawaib. (Nao ni ngamia walioachiliwa huru kwa sababu ya masanamu yao.) Na Haam (yani ngamia wa kiume anayezalisha wanangamia kumi, hivyo akaachiliwa huru) na mfano wa hayo. Na yanaingia katika hilo pia kula vyakula vilivyoharamishwa. “Hakika yeye ni adui yenu aliye dhahiri.” Yani mwenye uadui wa dhahiri, hivyo hataki katika kuuamrisheni isipokuwa kuwapunja, na kwamba muwe miongoni mwa wa wenza wa Moto mkali. Na Mola wetu Mlezi hakutoshea katika kutukaza tu kufuata nyayo zake. Mpaka alipotuambia – naye ndiye mkweli zaidi wa wale wanaosema - juu ya uadui wake unaotaka mtu kujitahadharisha naye. Kisha hakutoshea kwa hilo mpaka akatujulisha yale anayoamrisha kwa kina, na kwamba ndivyo vitu viovu zaidi, na vyenye uharibifu mkubwa zaidi, akasema: