البقرة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
ٱلْحَقُّ مِن رَّبِّكَ ۖ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلْمُمْتَرِينَ ١٤٧
(147) “Haki inatoka kwa Mola wako Mlezi.” Yani haki hii ambayo inastahiki zaidi kuitwa haki kuliko kila kitu, kwa sababu ya kile kinachojumuisha cha mahitaji makubwa, maamrisho mazuri, utakaso wa nafsi na kuzihimiza kutafuta masilahi yake. Na kuzuia yenye kuziharibu kwa sababu, imetoka kwa Mola wako Mlezi ambaye katika jumla ya malezi yake kwako ni kwamba alikuteremshia Qur-ani hii juu yako. Ambayo ndani yake kuna malezi ya akili na nafsi, na masilahi yote. “Basi usiwe kabisa miongoni mwa wenye shaka.” Yani isikupate hata chembe ndogo mno ya shaka na kusitasita juu yake. Bali tafakari juu yake na uangalie kwa makini mpaka upate yakini kwa hayo. Kwa sababu, kutafakari juu yake, bila shaka kunazuia shaka na kunafikisha kwenye yakini.