مريم
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
أَطَّلَعَ ٱلْغَيْبَ أَمِ ٱتَّخَذَ عِندَ ٱلرَّحْمَـٰنِ عَهْدًا ٧٨
{78} Mwenyezi Mungu akasema kwa kumkemea na kumkadhibisha, "Kwani yeye amepata habari za ghaibu?" Yaani, elimu yake iliizunguka ghaibu mpaka akajua yatakayotokea, na kwamba miongoni mwa mambo yatakayotokea ni kuwa atapewa mali na watoto Siku ya Qiyama? "Au amechukua ahadi kwa Arrahmani (Mwingi wa Rehema)" ya kwamba atapata aliyoyasema? Yaani, hakuna lolote kati ya hayo lililotokea. Kwa hivyo ikajulikana kwamba anazua tu maneno haya, na kusema mambo ambayo hana elimu yoyote nayo. Na kugawanya huku na kurejea ni katika mbinu kubwa zaidi ziwezekanazo katika kulazimisha na kumsimamishia hoja. Kwani mwenye kudai kuwa atapata heri kwa Mwenyezi Mungu huko Akhera hatoki katika hali hizi. Ima kauli yake hiyo inatokana na kujua kwake ghaibu ya mambo yajayo, na tayari ilikwisha julikana kwamba hayo ni ya Mwenyezi Mungu peke yake. Kwa hivyo, hakuna yeyote ajuaye mambo ya ghaibu isipokuwa yale ambayo Mwenyezi Mungu aliwajulisha Mitume wake. Au iwe kwamba alichukua ahadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu ya kumwamini na kuwafuata Mitume wake, ambao Mwenyezi Mungu aliwaahidi wafanyao hivyo na akafunua kwamba hao ndio wenye kupata akhera, ambao wataokoka na kufaulu. Na mambo haya mawili yasipopatikana, basi inajulikana kwamba madai hake hayo ni batili.