مريم
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
يَـٰزَكَرِيَّآ إِنَّا نُبَشِّرُكَ بِغُلَـٰمٍ ٱسْمُهُۥ يَحْيَىٰ لَمْ نَجْعَل لَّهُۥ مِن قَبْلُ سَمِيًّا ٧
{7} Yaani, Mwenyezi Mungu Mtukufu alimpa bishara njema kupitia Malaika kuhusu kuzaliwa kwa Yahya, na Mwenyezi Mungu mwenyewe ndiye aliyempa jina la Yahya, nalo lilikuwa jina lanalolingana na yule aliyeitwa kwalo. Yaani, atakuwa na uhai kwa kihisia, ndiyo iwe neema hivyo imetimia sawasawa. Na kwamba pia ataishi usio kuwa wa kihisia ambao ni uhai wa moyo na roho kwa wahyi, elimu na Dini. "Hatujapata kumpa jina hilo yeyote kabla yake." Na pia maana yake inaweza kuwa: Hatukuwahi kumfanya yeyote kuwa mfano wake na sawa naye. Ndiyo hiyo iwe ni bishara njema hukusu ukamilifu wake na kusifika kwake kwa sifa nzuri, na kwamba anawashinda waliokuwa kabla yake. Lakini kulingana na maana hii, ujumla huu lazima atolewe ndani yake Ibrahim, Musa, na Nuhu amani iwe juu yao na mfano wao, miongoni mwa wale ambao ni bora zaidi ya Yahya bila shaka yoyote.