انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · مريم
السورة ١٩

مريم

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٦٢

لَّا يَسْمَعُونَ فِيهَا لَغْوًا إِلَّا سَلَـٰمًا ۖ وَلَهُمْ رِزْقُهُمْ فِيهَا بُكْرَةً وَعَشِيًّا ٦٢

{62} "Humo hawatasikia upuuzi wowote" wala mambo yenye kumfanya mtu kuwa na dhambi. Kwa hivyo, hawatasikia humo matusi, wala kutilia kitu dosari, wala kauli ya kumuasi Mwenyezi Mungu, au maneno ya kuhuzunisha "isipokuwa Salama tu." Yaani, [isipokuwa] kauli ambazo ni salama kutokana na dosari yoyote. Humo kutakuwa tu na kumtaja Mwenyezi Mungu, na maamkizi, na maneno ya furaha na bishara njema, mazungumzo mazuri kati ya ndugu, kusikia muzungumzo ya Mwingi wa rehema, sauti za kupendeza za hurulaini, malaika na watoto wadogo, nyimbo za kupendeza mno, na maneno mazuri. Kwa sababu nyumba hiyo ni nyumba yenye salama. Hakuna ndani yake isipokuwa usalama kamili katika njia zote. "Na watapata humo riziki zao" miongoni mwa vyakula, vinywaji, na aina mbalimbali za starehe "asubuhi na jioni." Yaani, zitaendelea popote pale watakapoomba na wakati wowote watakapotaka. Na katika ukamilifu wake, raha yake, na uzuri wake ni kwamba zitakuwa katika nyakati zinazojulikana, asubuhi na jioni. Ili kuongeza athari vikubwa na yatimie manufaa yake.