مريم
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
أُو۟لَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ أَنْعَمَ ٱللَّهُ عَلَيْهِم مِّنَ ٱلنَّبِيِّـۧنَ مِن ذُرِّيَّةِ ءَادَمَ وَمِمَّنْ حَمَلْنَا مَعَ نُوحٍ وَمِن ذُرِّيَّةِ إِبْرَٰهِيمَ وَإِسْرَٰٓءِيلَ وَمِمَّنْ هَدَيْنَا وَٱجْتَبَيْنَآ ۚ إِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ ءَايَـٰتُ ٱلرَّحْمَـٰنِ خَرُّوا۟ سُجَّدًا وَبُكِيًّا ۩ ٥٨
{58} Alipowataja Manabii hawa watukufu, na Mitume maalumu na akataja fadhila na daraja zao, akasema, "Hao ndio aliowaneemesha Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii." Yaani, Mwenyezi Mungu aliwaneemesha kwa neema isiyoweza kufikiwa wala kupitwa kama vile unabii na utume. Na hao ndio tuliamrishwa kwamba tumuombe Mwenyezi Mungu atuongoe kwenye njia ya wale aliowaneemesha, na kwamba mwenye kumtii Mwenyezi Mungu, atakuwa “pamoja na wale ambao Mwenyezi Mungu amewaneemesha miongoni mwa manabii...” hadi mwisho wa Aya. Na kwamba baadhi yao ni “uzao wa Adam, na katika uzao wa wale tuliowabeba pamoja na Nuhu.” Yaani, kutoka katika kizazi chake. "Na katika uzao wa Ibrahim na Israil." Hizi ndizo nyumba bora zaidi katika walimwengu wote. Mwenyezi Mungu aliwateua na kuwachagua, na ilikuwa hali yao pale wanaposomewa Aya za Mwingi wa rehema, zilizojumuisha habari za ghaibu na sifa za Ajuaye zaidi ghaibu, na habari za Siku ya Mwisho, na ahadi nzuri na ahadi ya adhabu kali, "huanguka kusujudu na kulia." Yaani, walikuwa wakizinyenyekea Aya za Mwenyezi Mungu, na zikawa zinaathiri katika nyoyo zao kwa kuwapa imani, kumtaka Mwenyezi Mungu na kumhofu, mambo yaliyowasababishia kulia, kurudi kwa Mwenyezi Mungu, na kumsujudia Mola wao Mlezi, na hawakuwa miongoni mwa wale ambao walipozisikia Aya za Mwenyezi Mungu, wanajifanya viziwi nazo na vipofu. Na katika kufungamanisha Aya na jina lake, Mwingi wa rehema, kuna ushahidi Aya zake ni katika rehema zake na ihsani yake kwa waja wake, ambapo aliwaongoa kwazo kwenye haki, akawafanya kuona kutokana na kuwa na upofu, akawaokoa kutoka katika upotovu, na akawafundisha baada ya kwamba walikuwa wajinga.