مريم
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَٱذْكُرْ فِى ٱلْكِتَـٰبِ إِسْمَـٰعِيلَ ۚ إِنَّهُۥ كَانَ صَادِقَ ٱلْوَعْدِ وَكَانَ رَسُولًا نَّبِيًّا ٥٤
{54} Yaani, mtaje katika Qur-ani Tukufu nabii huyu mkuu, ambaye taifa la Kiarabu lilitokana naye, ambalo ndilo taifa bora na tukufu zaidi. Ambalo ametokana nalo bwana wa mwana wa Adam. "Bila ya shaka yeye alikuwa ni mkweli wa ahadi." Yaani, hakuwa akitoa ahadi yoyote isipokuwa anaitekeleza kikamilifu. Na hili linajumuisha ahadi anayoifunga na Mwenyezi Mungu au anayoifunga na waja wake. Na ndiyo maana alipojiahidi kuwa na subira baba yake alipotaka kumchinja, akasema, "utanikuta mimi, Inshallah (Mwenyezi Mungu akipenda), katika wanaosubiri." Akalitimiza hilo, na akamuwezesha baba yake kwamba amchinje, jambo ambalo ndilo msiba mkubwa zaidi unaoweza kumsibu mtu. Kisha akamsifia kwa sifa ya utume na unabii ambayo ndiyo neema kubwa zaidi za Mwenyezi Mungu juu ya mja wake, na akamfanya kuwa miongoni mwa viumbe wa daraja la juu kabisa.