مريم
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَٱذْكُرْ فِى ٱلْكِتَـٰبِ مُوسَىٰٓ ۚ إِنَّهُۥ كَانَ مُخْلَصًا وَكَانَ رَسُولًا نَّبِيًّا ٥١
{51} Yaani, mtaje katika Qur-ani hii tukufu Musa mwana wa Imran kwa njia ya kumtukuza, na kumpa taadhima, na kujulisha cheo chake kitukufu na tabia zake zilizokamilika. "Hakika yeye alikuwa ni mwenye kuchaguliwa." Na ilisomwa (mukhlaswan) kwa kutia fatḥa kwenye lam, nalo ni lenye maana ya kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu alimteua, akamchagua juu ya walimwengu wote. Na likasomwa neno hilo kwa kasra, nalo ni lenye maana ya kwamba yeye ni "mwenye kumkusudia tu" Mwenyezi Mungu Mtukufu katika matendo yake yote, na maneno yake, na makusudio yake. Kwa hivyo akamsifu kwamba alikuwa akimkusudia Yeye tu katika hali zake zote. Na maana hizi mbili hazitenganishwi. Kwa maana, Mwenyezi Mungu alimteua kwa sababu yeye Musa alikuwa akimkusudia Yeye tu. Nako kumkusudia kwake huku kunalazimu kuchaguliwa kwake. Na hali bora zaidi ambayo mja anaweza kuelezewa nayo ni yeye kumkusudia tu Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu kumteua. "Na alikuwa ni Mtume, Nabii." Yaani, Mwenyezi Mungu alimuunganishia utume na unabii. Na utume unahitaji kufikisha maneno ya mtumaji, na kufikisha yale yote aliyoyaleta ya Sheria, madogo yake na makubwa yake. Nao unabii unahitaji kwamba Mwenyezi Mungu alimfunulia wahyi, na kumteua yeye tu kwa ufunuo huo. Basi unabii huwa baina yake na Mola wake Mlezi, nao utume huwa baina yake na viumbe.