مريم
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
فَٱتَّخَذَتْ مِن دُونِهِمْ حِجَابًا فَأَرْسَلْنَآ إِلَيْهَا رُوحَنَا فَتَمَثَّلَ لَهَا بَشَرًا سَوِيًّا ١٧
{17} "Na akaweka pazia kujikinga nao " ili asalie peke yake kwa ajili ya kumuabudu Mola wake Mlezi katika hali ya unyenyekevu na udhalilifu kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na hilo ni kwa ajili ya kutekeleza kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu. "Na angalia pale Malaika waliposema: Ewe Maryamu! Kwa hakika Mwenyezi Mungu amekuteua, na akakutakasa, na akakutukuza kuliko wanawake wa walimwengu wote." Ewe Maryamu! Mnyenyekee Mola wako Mlezi na usujudu na uiname pamoja na wainamao." Na kauli yake, "Basi tukamtumia Roho wetu" naye ni Jibril, amani iwe juu yake, "naye akajifananisha kwake sawa sawa na mtu." Yaani, mwanamume mkamilifu katika sura nzuri na mwonekano mzuri bila ya kuwa na dosari yoyote wala upungufu, kwa sababu hawezi Maryamu kuvumilia kumwona jinsi alivyo.