مريم
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
يَـٰيَحْيَىٰ خُذِ ٱلْكِتَـٰبَ بِقُوَّةٍ ۖ وَءَاتَيْنَـٰهُ ٱلْحُكْمَ صَبِيًّا ١٢
{12} Maneno yaliyotangulia yaonyesha kuzaliwa kwa Yahya, ujana wake na malezi yake. Alipofikia hali ambapo anayaelewa maneno vizuri, Mwenyezi Mungu alimwamrisha achukue kitabu hicho kwa nguvu. Yaani, kwa kujitahidi katika kuhifadhi maneno yake na kufahamu maana yake na kufanyia kazi maamrisho yake na makatazo yake. Huku ndiko kuchukua kitabu kwa ukamilifu. Kwa hivyo, akatekeleza amri ya Mola wake Mlezi. Akakichukua kitabu hicho na akakihifadhi na kukielewa, na Mwenyezi Mungu akampa werevu na utambuzi mkubwa ambao haukupatikana asiyekuwa yeye. Na ndiyo maana akasema, "Nasi tulimpa hekima angali mtoto" [Yaani, kuzijua hukumu za Mwenyezi Mungu na kuhukumu kwazo hali ya kuwa bado angali mdogo].