الكهف
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَأَمَّا مَنْ ءَامَنَ وَعَمِلَ صَـٰلِحًا فَلَهُۥ جَزَآءً ٱلْحُسْنَىٰ ۖ وَسَنَقُولُ لَهُۥ مِنْ أَمْرِنَا يُسْرًا ٨٨
{88} "Na ama yule mwenye kuamini na akatenda mema, basi huyo ana malipo mazuri." Yaani, atapata Pepo na hali nzuri kwa Mwenyezi Mungu, yawe ndiyo malipo yake siku ya Qiyama. "Nasi tutamwambia lililo jepesi katika amri yetu." Yaani, tutamtendea mazuri, na kusema naye kwa upole, na kuamiliana naye kwa urahisi. Na hili linaonyesha kwamba yeye ni miongoni mwa wafalme wema [na] vipenzi wa Mwenyezi Mungu waadilifu, wenye elimu, kwa maana aliafikiana na yanayomridhisha Mwenyezi Mungu katika kuamiliana na kila mtu kwa yale yanayoifailia hali yake.