الكهف
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
حَتَّىٰٓ إِذَا بَلَغَ مَغْرِبَ ٱلشَّمْسِ وَجَدَهَا تَغْرُبُ فِى عَيْنٍ حَمِئَةٍ وَوَجَدَ عِندَهَا قَوْمًا ۗ قُلْنَا يَـٰذَا ٱلْقَرْنَيْنِ إِمَّآ أَن تُعَذِّبَ وَإِمَّآ أَن تَتَّخِذَ فِيهِمْ حُسْنًا ٨٦
{86} Kwa hivyo Mwenyezi Mungu akampa kile alichofika kwacho "machweo ya jua," hadi akaliona jua kulingana na kuona kwa macho kana kwamba "linatua katika chemchemi yenye matope meusi." Na hili ni la kawaida kwa yule ambaye kuna maji baina yake na upeo wa jua wa magharibi. Aliliona likitua katika maji hayo, hata ingawa lilikuwa limeinuka juu sana. "Na pale akawakuta kaumu fulani. Tukasema: Ewe Dhul-Qarnain, ima uwaadhibu" kwa kuwaua, au kuwapiga, au kuwateka au mfano wake, "au uwafanyie uzuri." Kwa hivyo akapewa chaguo kati ya mambo hayo mawili. Kwa sababu, ilionekana kwa dhahiri kwamba wao [ima] ni makafiri au watu wavukao mipaka au ndani yao kuna mambo kama hayo. Kwa sababu wangekuwa waumini wasiovuka mipaka, basi asingeruhusiwa kuwaadhibu.