انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الكهف
السورة ١٨

الكهف

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٥٢

وَيَوْمَ يَقُولُ نَادُوا۟ شُرَكَآءِىَ ٱلَّذِينَ زَعَمْتُمْ فَدَعَوْهُمْ فَلَمْ يَسْتَجِيبُوا۟ لَهُمْ وَجَعَلْنَا بَيْنَهُم مَّوْبِقًا ٥٢

{52} Na alipotaja hali ya wanaomshirikisha duniani, na akaibatilisha kabisa shirki hii, na akahukumu kwamba mwenye hayo ni mjinga na mpumbavu, akajulisha kuhusu hali yao kwa washirika wao Siku ya Qiyama, na kwamba Mwenyezi Mungu atawaambia: Waiteni washirika wangu - kulingana na madai yenu mabovu, Vinginevyo, ukweli ni kwamba Mwenyezi Mungu hana mshirika yeyote katika ardhi wala mbinguni. Yaani, waiteni ili wawanufaishe na wawaepushe na magumu. "Basi watawaita, na wao hawatawaitikia." Kwa sababu hukumu na ufalme siku hiyo ni wa Mwenyezi Mungu, na hakuna yeyote atakayemiliki manufaa uzito wa chembe kwa ajili yake mwenyewe wala kwa ajili ya mwingine. "Na tutaweka baina yao;" yaani, baina ya washirikina na washirika wao "maangamio", yatakayowatenganisha wao kwa wao, na kuwaweka mbali wao kwa wao, na wakati huo utabainika uadui wa washirika kwa washirika wao, na kuwakufuru kwao, na kuijitenga kwao nao. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Na watakapokusanywa watu, watakuwa maadui zao wataikufuru ibada yao."