انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الكهف
السورة ١٨

الكهف

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٤٩

وَوُضِعَ ٱلْكِتَـٰبُ فَتَرَى ٱلْمُجْرِمِينَ مُشْفِقِينَ مِمَّا فِيهِ وَيَقُولُونَ يَـٰوَيْلَتَنَا مَالِ هَـٰذَا ٱلْكِتَـٰبِ لَا يُغَادِرُ صَغِيرَةً وَلَا كَبِيرَةً إِلَّآ أَحْصَىٰهَا ۚ وَوَجَدُوا۟ مَا عَمِلُوا۟ حَاضِرًا ۗ وَلَا يَظْلِمُ رَبُّكَ أَحَدًا ٤٩

{49} Kisha wakati huo vitaletwa vitabu vya matendo vilivyoandikwa na Malaika wema. Na mioyo itawaruka kwa sababu yake, na dhiki itakuwa kubwa mno kwa sababu yake, na utakaribia uziwi mgumu kuyeyuka, na wahalifu wataviogopa mno. Na wanapoona kwamba yameandikwa humo matendo yao, yemedhibitiwa maneno yao na vitendo vyao, watasema, “Ole wetu! Kitabu hiki kina nini! Hakiachi dogo wala kubwa isipokuwa hulidhibiti.” Yaani, hakiachi dhambi, dogo wala kubwa, isipokuwa liliandikwa humo na kuhifadhiwa, hakuna siri wala tendo lolote la hadharani wala la usiku wala mchana lililosahaulika. "Na watayakuta yote waliyoyatenda yapo hadharani," hawataweza kuyakanusha. "Na Mola wako Mlezi hamdhulumu yeyote." Basi wakati huo watalipwa kwayo na watafanywa kuyakubali, na watafedheheshwa na itawadhibitikia adhabu. "Hayo ni kwa yale iliyotanguliza mikono yao, na kwamba Mwenyezi Mungu si mwenye kuwadhulumu waja wake." Bali hawakutoka katika uadilifu wake na fadhila zake.