الكهف
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
إِلَّآ أَن يَشَآءَ ٱللَّهُ ۚ وَٱذْكُر رَّبَّكَ إِذَا نَسِيتَ وَقُلْ عَسَىٰٓ أَن يَهْدِيَنِ رَبِّى لِأَقْرَبَ مِنْ هَـٰذَا رَشَدًا ٢٤
{24} Na kwa vile mja ni mtu, na hana budi kusahau kutaja mapenzi ya Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu akamuamuru kulitaja anapokumbuka baada ya hilo, ili kinachotarajiwa kipatikane na kilichotahadhariwa kiondoke. Na imechukuliwa katika ujumla wa kauli yake, "Na mkumbuke Mola wako Mlezi pale unaposahau" amri ya kumdhukuru Mwenyezi Mungu unaposahau. Kwa maana, hilo humkumbusha mja yale aliyoyasahau. Vilevile yule aliyesahau kumkumbuka Mwenyezi Mungu ameamrishwa amdhukuru Mola wake Mlezi wala kamwe asiwe miongoni mwa walioghafilika. Na kwa vile mja humhitajia zaidi Mwenyezi Mungu ili awezeshwe kufikia usawa na asikosee katika maneno yake na vitendo vyake, Mwenyezi Mungu alimuamuru aseme, “Huenda Mola wangu Mlezi ataniongoa kwenye uwongozi ulio karibu zaidi kuliko huu.” Basi akamuamuru kuomwomba Mwenyezi Mungu, na amtarajie, na awe na imani naye kwamba atamwongoa kwenye njia iliyo karibu zaidi ifikishayo kwenye uwongofu. Basi inamfailia zaidi mja ambaye hii ndiyo hali yake, kisha akafanya juhudi, na akafanya awezavyo katika kutafuta uwongofu na usawa, kwamba huwezeshwa kuyafikia hayo, na hujiwa na msaada kutoka kwa Mola wake Mlezi, na kwamba Mola wake Mlezi humuweka sawasawa katika mambo yake yote.