الكهف
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَإِذِ ٱعْتَزَلْتُمُوهُمْ وَمَا يَعْبُدُونَ إِلَّا ٱللَّهَ فَأْوُۥٓا۟ إِلَى ٱلْكَهْفِ يَنشُرْ لَكُمْ رَبُّكُم مِّن رَّحْمَتِهِۦ وَيُهَيِّئْ لَكُم مِّنْ أَمْرِكُم مِّرْفَقًا ١٦
{16} Yaani wao kwa wao wakaambiana: Mkijitenga na kaumu yenu kwa miili yenu na dini zenu, basi haitabakia isipokuwa kuokoka kutokana na uovu wao na kufanya sababu zenye kusababisha hayo. Kwa sababu hawana njia yoyote ya kupigana nao wala kubakia miongoni mwao ilhali hawaifuati dini yao. "Basi kimbilieni pangoni" mjifiche humo "awafungulie Mola wenu Mlezi katika rehema zake, na awatengenezee ya kuwafaa katika mambo yenu." Na katika yaliyotangulia alijulisha kuwa wao walimuomba kwa kusema, "Mola wetu Mlezi! Tupe rehema itokayo kwako, na tutengezee uwongofu katika jambo letu." Basi wakajumuisha kati ya kujitenga na uwezo wao na nguvu zao, na kukimbilia kwa Mwenyezi Mungu ili awatengenezee mambo yao na wamuombe hayo, na kati ya kuwa na imani na Mwenyezi Mungu kwamba atafanya hivyo. Hakuna shaka kwamba Mwenyezi Mungu aliwafungulia katika rehema zake na akawatengenezea ya kuwafaa katika mambo yao. Basi akazihifadhi dini zao na miili yao, na akawafanya kuwa miongoni mwa ishara zake kwa viumbe vyake, na akawaeneza sifa nzuri jambo ambalo ni katika rehema yake kwao, na akawasahilishia kila njia, hata mahali walipokuwa wakilala palikuwa na kuhifadhiwa kwa hali ya juu zaidi iwezekanayo. Na ndiyo maana akasema: