انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الكهف
السورة ١٨

الكهف

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١١٠

قُلْ إِنَّمَآ أَنَا۠ بَشَرٌ مِّثْلُكُمْ يُوحَىٰٓ إِلَىَّ أَنَّمَآ إِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَٰحِدٌ ۖ فَمَن كَانَ يَرْجُوا۟ لِقَآءَ رَبِّهِۦ فَلْيَعْمَلْ عَمَلًا صَـٰلِحًا وَلَا يُشْرِكْ بِعِبَادَةِ رَبِّهِۦٓ أَحَدًۢا ١١٠

{110} Yaani, waambie ewe Muhammad makafiri na wegineo, "Hakika, mimi ni mwanadamu tu kama nyingi" na mimi si mungu, wala sina ushirika wowote katika ufalme wa Mwenyezi Mungu, wala sijui elimu ya ghaibu, wala sina hazina za Mwenyezi Mungu. Lakini mimi hakika ni mwanadamu tu kama nyinyi, na mja miongoni mwa waja wa Mola wangu Mlezi. "Ninaletewa Wahyi kwamba Mungu wenu ni Mungu Mmoja tu." Yaani, nimeboreshwa juu yenu kwa ufunuo ambao Mwenyezi Mungu ananifunulia mimi, ambao mkubwa wake zaidi ni kuwaambia kwamba, "Mungu wenu ni Mungu Mmoja tu" hana mshirika yeyote wala hakuna yeyote anayestahili kuabudu uzito wa chembe [isipokuwa yeye tu], na ninawaita kwenye matendo ambayo inawaleta karibu naye, kuwapa thawabu zake na inawaondolea adhabu yake. Na ndiyo maana akasema, "Kwa hivyo, mwenye kutaraji kukutana na Mola wake Mlezi, basi na atende matendo mema." Nayo ni yale matendo ambayo yanaafikiana na sheria ya Mwenyezi Mungu miongoni mwa mambo ya wajibu na yale yaliyopendekezwa. "Wala asimshirikishe yeyote katika ibada ya Mola wake Mlezi." Yaani, asijioneshe kwa matendo yake, lakini ayafanye kwa kuukusudia uso wa Mwenyezi Mungu Mtukufu tu. Basi huyu aliyeunganisha kati ya kumkusudia Mwenyezi Mungu tu na kufuata sheria ya sawasawa ndiye atakayepata kile anachotarajia na anachotafuta. Na ama asiyekuwa kama huyu, basi yeye amehasiri katika dunia yake na akhera yake, na ameshapoteza kuwa karibu na Mola wake na kupata radhi zake.

Mwisho wa Tafsiri ya Surat Al-Kahf. Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu.