الإسراء
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
قُلْ كَفَىٰ بِٱللَّهِ شَهِيدًۢا بَيْنِى وَبَيْنَكُمْ ۚ إِنَّهُۥ كَانَ بِعِبَادِهِۦ خَبِيرًۢا بَصِيرًا ٩٦
{96} "Sema: Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi baina yangu na nyinyi. Hakika Yeye ana habari zote za waja wake na anawaona vyema." Na katika ushahidi wake kwa Mtume wake ni miujiza aliyomsaidia nayo na Aya alizomteremshia, na nusura aliyompa dhidi ya wale waliomkaidi na kumfanyia uadui. Na lau kama angelimzulia baadhi ya maneno tu. Basi bila ya shaka angelimshika kwa mkono wa kulia. Kisha kwa hakika angelimkata mshipa mkubwa wa moyo! Kwani Yeye ni Mwenye habari zote, Mwenye kuona vyema, na hakuna chenye kufichika chochote kinachofichikana kwake kuhusu hali za waja wake.