الإسراء
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَيَسْـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلرُّوحِ ۖ قُلِ ٱلرُّوحُ مِنْ أَمْرِ رَبِّى وَمَآ أُوتِيتُم مِّنَ ٱلْعِلْمِ إِلَّا قَلِيلًا ٨٥
{85} Hili linajumusiha kumkomesha mwenye kuuliza maswali ambayo hayakusudiwi kwayo isipokuwa ukaidi na kutaka kumshinda aliyeulizwa, na akaacha kuuliza yaliyo muhimu. Hao waliuliza kuhusu roho, ambayo ni katika mambo yaliyofichika ambayo kila mmoja hawezi kuielezea namna ilivyo kihalisia, ilhali hata wana upungufu mkubwa katika elimu wanayohitaji waja kuijua. Na ndiyo maana Mwenyezi Mungu akamwamrisha Mtume wake kulijibu swali lao kwa kauli yake, “Sema: Roho ni katika mambo ya Mola wangu Mlezi.” Yaani, ni katika jumla ya viumbe vyake aliowaamrisha wawe, na ikawa. Basi hakuna faida kubwa katika kuuliza juu yake, pamoja na kutojua kwenu mengineyo. Na Aya hii ina ushahidi kwamba anayeulizwa akiulizwa kuhusu jambo ambalo ilikuwa bora kwa mtu kuuliza juu ya jambo linginelo, basi na ampuuze wala asimjibu, na amuelekeze kwenye yale anayoyahitaji, na amuongoze katika yale yatakayomnufaisha.