الإسراء
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
أَقِمِ ٱلصَّلَوٰةَ لِدُلُوكِ ٱلشَّمْسِ إِلَىٰ غَسَقِ ٱلَّيْلِ وَقُرْءَانَ ٱلْفَجْرِ ۖ إِنَّ قُرْءَانَ ٱلْفَجْرِ كَانَ مَشْهُودًا ٧٨
{78} Yeye Mtukufu anamwamrisha Mtume wake Muhammad -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - kusimamisha Swala kamili, kwa dhahiri na kwa siri katika nyakati zake zilizowekwa, "jua linapopinduka." Yaani, linapoelekea kwenye upeo wa magharibi baada ya kukengeuka kwake. Na inaingia katika hilo swala ya adhuhuri na swala ya alasiri "mpaka giza la usiku." Na inaingia katika hilo swala ya Maghribi na swala ya Ishaa, "Na Qur-rani ya Al-fajiri." Yaani, swala ya alfajiri. Nayo iliitwa Qur-ani kwa sababu inaruhusiwa kurefusha kisomo cha Qur-ani ndani yake kuliko swala zinginezo, na kwa sababu ya fadhila ya kusoma Qur-ani, ambacho Mwenyezi Mungu anakishuhudia, na Malaika wa usiku na Malaika wa mchana. Basi katika Aya hii zimetajwa nyakati tano za swala tano za faradhi zilizoandikwa, na kwamba zinazofanywa nyakati hizo ni faradhi, kwa sababu ya kutajwa hizo tu katika amri hii. Na ndani yake pia kuna kwamba kuingia kwa wakati ni sharti ya swala kuwa sahihi, na kwamba ndiyo sababu ya kuifanya iwe wajibu. Kwa sababu Mwenyezi Mungu aliamuru kuisimamisha katika nyakati hizi. Na ndani yake pia kuna kwamba Adhuhuri na Alasiri huchanganywa pamoja, na Magharibi na Ishaa pia huchanganywa pamoja kama kuna udhuru wa kufanya hivyo. Kwa sababu Mwenyezi Mungu alijumuisha nyakati zake pamoja. Na ndani yake pia kuna fadhila ya swala ya Alfajiri, na fadhila ya kurefusha kisomo cha Qur-ani ndani yake, na kwamba kusoma Qur-ani ndani yake ni nguzo yake. Kwa sababu ikiwa ibada itaitwa kwa baadhi ya sehemu zake, basi hilo litaonyesha ulazima wa sehemu hiyo.