انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الإسراء
السورة ١٧

الإسراء

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٥٩

وَمَا مَنَعَنَآ أَن نُّرْسِلَ بِٱلْـَٔايَـٰتِ إِلَّآ أَن كَذَّبَ بِهَا ٱلْأَوَّلُونَ ۚ وَءَاتَيْنَا ثَمُودَ ٱلنَّاقَةَ مُبْصِرَةً فَظَلَمُوا۟ بِهَا ۚ وَمَا نُرْسِلُ بِٱلْـَٔايَـٰتِ إِلَّا تَخْوِيفًا ٥٩

{59} Yeye Mtukufu anataja rehema yake ya kutoteremsha ishara wanazopendekeza hao wanaokadhibisha, na kwamba halikumzuia Yeye kuzituma isipokuwa kwa kuhofia waje kuzikadhibisha. Na wakizikadhibisha, adhabu inawapata haraka bila ya kuchelewa, kama ilivyowafanya wa mwanzo ambao walizikadhibisha. Na miongoni mwa ishara kubwa zaidi ni ile ishara aliyoituma Mwenyezi Mungu kwa Thamud, ambaye ni ngamia jike mkubwa mwenye kung’aa sana, ambaye kabila zima lilikuwa linakunywa maziwa kutoka kwake lakini wakaikadhibisha ishara hiyo, basi wakapatwa na yale aliyotuhadithia Mwenyezi Mungu katika Kitabu chake. Na hawa pia, lau zitawajia ishara kubwa kubwa, hawataamini. Kwa maana, hakikuwazuia kuamini kuficha kwa yale waliyokuja nayo Mtume na kuchanganyika kwake: ni haki au batili? Kwani zimekuja hoja nyingi zinazoashiria usahihi wa yale aliyowajia nayo, jambo lanalosababisha aongoke anayetafuta uwongofu, na ishara zinginezo ni mfano wa hizo tu, na ni lazima watazitendea kama walivyozitendea zinginezo. Kwa hivyo kuacha kuziteremsha ilhali hii ndiyo hali, ni bora kwao na ni la manufaa zaidi. Na kauli yake, “Nasi hatutumi Ishara isipokuwa kwa ajili ya kuhadharisha.” Yaani, hazikukusudiwa kuwa sababu ya kuamini kwao ambako hakuwezi kupatikana bila ya hizo, bali zilikusudiwa kuhofisha na kutishia, ili wakomeke na yale waliyonayo.