انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الإسراء
السورة ١٧

الإسراء

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٥٧

أُو۟لَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ يَدْعُونَ يَبْتَغُونَ إِلَىٰ رَبِّهِمُ ٱلْوَسِيلَةَ أَيُّهُمْ أَقْرَبُ وَيَرْجُونَ رَحْمَتَهُۥ وَيَخَافُونَ عَذَابَهُۥٓ ۚ إِنَّ عَذَابَ رَبِّكَ كَانَ مَحْذُورًا ٥٧

{57} Kisha akajulisha pia kwamba wao wanawaabudu badala ya Mwenyezi Mungu wako katika shughuli inayowafanya kuwasahau kwa sababu wanajali sana uhitaji wao kwa Mwenyezi Mungu na kutafuta njia ya kumfikia. Akasema, “Hao ambao wao wanaowaomba” miongoni mwa Manabii, watu wema, na Malaika, "wao wenyewe wanatafuta njia ya kwendea kwa Mola wao Mlezi hata miongoni mwao walio karibu mno." Yaani, wanashindana katika kuwa karibu na Mola wao Mlezi, na wanafanya yale wanayoweza miongoni mwa matendo mema ambayo yatawaweka karibu na Mwenyezi Mungu Mtukufu na rehema zake, "na wanaihofu adhabu yake" basi wanajiepusha na kila kitu chenye kufikisha kwenye adhabu yake. "Hakika adhabu ya Mola wako Mlezi yafaa kutahadhariwa" na kujiepusha na sababu zake. Na mambo haya matatu: hofu, matumaini, na upendo, ambayo Mwenyezi Mungu aliwaelezea hawa walio karibu naye, ndiyo msingi na kiini cha heri yote. Kwa hivyo, aliye nayo, basi mambo yake yanakuwa yamekamilika. Na ikiwa moyo hautakuwa nayo, basi heri zinauondoka, na unazungukwa na maovu. Na alama ya upendo ni kama alivyotaja Mwenyezi Mungu kwamba mja ajitahidi katika kila tendo linalomkurubisha kwa Mwenyezi Mungu, na kushindana katika kujikurubisha kwake kwa kumtaka Mwenyezi Mungu tu katika matendo yote, kuyafanya kuwa safi na kuyatekeleza kwa njia ya ukamilifu zaidi iwezekanayo. Kwa hivyo, mwenye kudai kwamba anampenda Mwenyezi Mungu na akafanya yasiyokuwa haya, basi yeye ni mwongo.