الإسراء
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَقَالُوٓا۟ أَءِذَا كُنَّا عِظَـٰمًا وَرُفَـٰتًا أَءِنَّا لَمَبْعُوثُونَ خَلْقًا جَدِيدًا ٤٩
{49} Mwenyezi Mungu Mtukufu anajulisha kuhusu maneno ya wanaokanusha kufufuliwa na kukadhibisha kwao hilo na kuona kwao kwamba hilo haliwezekani kwa kusema, "Tutakapokuwa mifupa na mapande yaliyovurugika." Yaani, miili iliyochakaa. "Tutafufuliwa kwa umbo jipya." Yaani, hilo halitatokea, na kwamba haliwezekani kulingana na madai yao, kwa hivyo ni wajinga mno. Ambapo waliwakadhibisha Mitume wa Mwenyezi Mungu, wakazikataa ishara za Mwenyezi Mungu, na wakapima uwezo wa Muumba wa mbingu na ardhi kwa uwezo wao dhaifu na usioweza kitu, na walipoona hawaliwezi hilo, wakaufanya uwezo wa Mwenyezi Mungu kuwa hivyo. Lakini ametakasika yule aliyewafanya viumbe miongoni mwa viumbe wake, ambao wanadai kuwa wao ndio wenye akili na ufahamu kuwa ni mfano wa kutojua mambo yaliyo dhahiri kabisa, na ya peupe yake zaidi, na yaliyo wazi yake zaidi kwa hoja, ili kuwaonyesha waja wake kwamba hakuna kufaulu isipokuwa kwa kuwezesha kwake, na usaidizi wake au kuangamia na kupotea. "Mola wetu Mlezi! Usizipotoe nyoyo zetu baada ya kwisha tuongoa, na utupe rehema itokayo kwako. Hakika Wewe ndiye Mwenye kutunuku."