الإسراء
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
نَّحْنُ أَعْلَمُ بِمَا يَسْتَمِعُونَ بِهِۦٓ إِذْ يَسْتَمِعُونَ إِلَيْكَ وَإِذْ هُمْ نَجْوَىٰٓ إِذْ يَقُولُ ٱلظَّـٰلِمُونَ إِن تَتَّبِعُونَ إِلَّا رَجُلًا مَّسْحُورًا ٤٧
{47} "Sisi tunajua vyema kabisa sababu wanayosikilizia." Yaani, tuliwazuia wasinufaike wanaposikia Qur-ani kwa sababu tunajua kwamba nia zao ni mbaya. Wanataka waone jambo dogo tu ili waikashifu. Kwa hivyo kusikiliza kwao huko si kwa ajili ya kutafuta mwongozo na kuikubali haki. Lakini wamekusudia kutokuifuata. Na yule ambaye hali yake ni hii, basi hawezi kunufaika na kitu katika kuisikiliza, na ndiyo sababu akasema, "wanapokusikiliza, na wanaponong'ona. Wanaposema hao madhalimu" katika kunong'ona kwao, "Nyinyi hamumfuati isipokuwa mwanamume aliyerogwa." Kwa hivyo, ikiwa huku ndiko kunong'onezana kwao kwa kidhalimu, na tayari walikujenga juu ya itikadi yao kwamba amefanyiwa uchawi, basi wameshakata shauri kwamba hawatayazingatia ayasemayo, na kwamba anaropokwa tu na hajui anachosema.