الإسراء
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَلَا تَقْرَبُوا۟ مَالَ ٱلْيَتِيمِ إِلَّا بِٱلَّتِى هِىَ أَحْسَنُ حَتَّىٰ يَبْلُغَ أَشُدَّهُۥ ۚ وَأَوْفُوا۟ بِٱلْعَهْدِ ۖ إِنَّ ٱلْعَهْدَ كَانَ مَسْـُٔولًا ٣٤
{34} Na hili ni katika upole wake na rehema yake kwa yatima yule ambaye alipoteza baba yake hali ya kuwa ni mdogo na bado hajajua masilahi yake mwenyewe na hata hawezi kuyatekeleza. Basi akamuamuru wasimamizi wake kumhifadhi na kuhifadhi mali yake na kuitengeneza, na kwamba wasiikaribie, "isipokuwa kwa kilicho kizuri zaidi" kama vile kuifanyia biashara, kutotia katika mambo hatari, na kufanya bidii ya kuikuza, na hayo yanafaa kuendelea hadi yatima atakapofikia "utu uzima wake." Yaani, atakapobaleghe na akapata akili komavu na akafanya mambo ya busara. Basi atakapofika utu uzima wake, ulezi ulio juu yake unaisha na anaweza sasa kujisimamia mwenyewe, na hapo atapewa mali yake. Kama alivyosema Yeye Mtukufu, "Mkiwaona ni werevu, basi wapeni mali yao." "Na kutimiza agano" ambalo mlimpa Mwenyezi Mungu, na ambayo mliagana na viumbe. "Kwa hakika ahadi itaulizwa juu yake." Yaani, mtaulizwa ikiwa mliitimiza au la. Kwa hivyo, ikiwa mlitimiza, basi mna thawabu nyingi. Na kama hamkufanya hivyo, basi mna dhambi kubwa.