انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الإسراء
السورة ١٧

الإسراء

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٨

مَّن كَانَ يُرِيدُ ٱلْعَاجِلَةَ عَجَّلْنَا لَهُۥ فِيهَا مَا نَشَآءُ لِمَن نُّرِيدُ ثُمَّ جَعَلْنَا لَهُۥ جَهَنَّمَ يَصْلَىٰهَا مَذْمُومًا مَّدْحُورًا ١٨

{18} Yeye Mtukufu anajulisha kwamba "anayetaka" dunia hii ambayo ni katika yale "yapitayo upesi upesi" itakayoisha na kuondoka, kwa hivyo akafanya matendo kwa ajili yake na akatia bidii katika hilo, na akasahau mwanzo au mwisho, basi Mwenyezi Mungu anamharakishia katika kumpa vitu vyake visivyo na thamani, na vitu vyake vinginevyo chochote anachopenda na anachotaka katika yale ambayo Mwenyezi Mungu alimwandikia katika Ubao Uliohifadhiwa, lakini ni vitu visivyo na manufaa wala vya kudumu navyo, na kisha amemuwekea katika Akhera, "Jahannamu; ataingia humo" na kukabiliana na adhabu yake, "hali ya kuwa ni mwenye kulaumiwa na kufurushwa." Yaani, katika hali ya hizaya, fedheha, na kashfa kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kutoka kwa viumbe vyake na kuwekwa mbali na rehema za Mwenyezi Mungu, kwa hivyo akawa amemjumuishia adhabu na fedheha.