الإسراء
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَكُلَّ إِنسَـٰنٍ أَلْزَمْنَـٰهُ طَـٰٓئِرَهُۥ فِى عُنُقِهِۦ ۖ وَنُخْرِجُ لَهُۥ يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ كِتَـٰبًا يَلْقَىٰهُ مَنشُورًا ١٣ ٱقْرَأْ كِتَـٰبَكَ كَفَىٰ بِنَفْسِكَ ٱلْيَوْمَ عَلَيْكَ حَسِيبًا ١٤
{13-14} Na huku ni kujulisha kuhusu ukamilifu wa uadilifu wake: kwamba kila mutu amemfungia matendo yake shingoni mwake. Yaani, matendo ya heri na maovu aliyokifanya, Mwenyezi Mungu atayafanya kuwa pamoja naye, hayatamruka yakamwendea mwingine. Kwa hivyo hatahesabiwa kwa matendo ya wengine, wala wengine hawatahesabiwa kwa matendo yake. "Na siku ya Qiyama tutamtolea kitabu atakachokutana nacho kimekunjuliwa," kikiwa na matendo yake ndani yake mema na maovu yamehudhuria, madogo na makubwa. Na ataambiwa, "Soma kitabu chako! Nafsi yako inakutosha leo kukuhesabu." Na hili ni katika uadilifu mkubwa zadi na haki, kwamba mja aambiwe, 'Jifanyie hesabu mwenyewe' ili apate kujua haki iliyo juu yake inayolazimu aadhibiwe.