انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · النحل
السورة ١٦

النحل

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٩٦

مَا عِندَكُمْ يَنفَدُ ۖ وَمَا عِندَ ٱللَّهِ بَاقٍ ۗ وَلَنَجْزِيَنَّ ٱلَّذِينَ صَبَرُوٓا۟ أَجْرَهُم بِأَحْسَنِ مَا كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ ٩٦

{96} Basi vipendeleeni vya kubakia juu ya vya kupotea. Kwa maana hakika vile, "Mlivyo navyo" - hata kama ni kingi namna gani - lazima vitakwisha na kutoweka. "Na vilivyo kwa Mwenyezi Mungu ndivyo vitakavyobakia" kwa kubakia kwake. Havitaisha wala havitapotea. Basi si mwenye akili atakayevipendelea vyenye kwisha visivyo na thamani juu ya vyenye kubakia vyenye thamani. Na hii ni kama kauli yake yeye Mtukufu, "Lakini nyinyi mnapendelea uhai wa dunia! Na Akhera ndiyo bora na yenye kudumu zaidi." "Na vilivyoko kwa Mwenyezi Mungu ndivyo bora kwa walio wema." Na hili limo himizo na kutia moyo juu ya kujitenga na dunia, hasa kujitenga ambako ni lazima, kama vile kujitenga na yale yenye kumdhuru mja na yenye kumfanya kujishughulisha na kuacha yale ambayo Mwenyezi Mungu alimuwajibishia na kuyatanguliza mbele ya haki ya Mwenyezi Mungu. Basi huku ndiko kujitenga na dunia ambako ni kwa wajibu. Na katika yale yenye kumsababishia mja kujitenga na dunia ni yeye kuzikabili starehe za dunia na matamanio yake kwa heri za Akhera. Kwani atapata tofauti kubwa kushindana kukubwa, jambo ambalo litamfanya kulipendelea jambo la juu zaidi kati ya mawili hayo. Na kujitenga na dunia kunakosifika si kujitenga ili kufanya ibada zinazomhusu mtu mwenyewe tu, kama vile swala, saum, dhikri, na mifano ya hayo. Bali hawi mja mwenye kujitenga na dunia kujitenga sahihi mpaka ayafanye yale awezayo miongoni mwa yale alioyoamrishwa kufanya miongoni mwa maamrisho ya kisheria ya wazi na ya ndani, na pia alinganie kwa Mwenyezi Mungu na kwa dini yake kwa kauli na vitendo. Na kujitenga na dunia ambako kwa hakika ni kujitenga na yasiyofaidi katika dini na dunia, na kuwa na utashi mkubwa, na kufanya bidii katika kila yenye kunufaisha, "Na kwa yakini Sisi tutawapa wale waliosubiri" juu ya kumtii Mwenyezi Mungu na kujiepusha na kumuasi Yeye, na wakajitoa kabisa matamanio ya kidunia yenye kudhuru dini yao. "Ujira wao kwa bora zaidi ya yale waliyokuwa wakiyatenda." Uzuri mmoja kwa mara kumi mfano wake hadi mizidisho mara mia saba hadi mizidisho mingi, kwa sababu hakika Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa anayetenda mazuri.