انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · النحل
السورة ١٦

النحل

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٩١

وَأَوْفُوا۟ بِعَهْدِ ٱللَّهِ إِذَا عَـٰهَدتُّمْ وَلَا تَنقُضُوا۟ ٱلْأَيْمَـٰنَ بَعْدَ تَوْكِيدِهَا وَقَدْ جَعَلْتُمُ ٱللَّهَ عَلَيْكُمْ كَفِيلًا ۚ إِنَّ ٱللَّهَ يَعْلَمُ مَا تَفْعَلُونَ ٩١

Na alipoamrisha yale ambayo ni wajibu katika asili ya sheria, akaamrisha kutimizwa kwa yale ambayo mja mwenyewe alijiwajibishia, akasema:

{91} Hii linajumuisha mambo yote ambayo mja alimuahidi Mola wake Mlezi miongoni mwa ibada mbalimbali kama vile nadhiri na viapo ambavyo mja alivifunga ikiwa kuna wema katika kuvitimiza. Na pia linajumuisha mikataba aliyofunga yeye na wengine, kama vile maagano wanayofanya wafanyao mikataba, na kama vile ahadi anayompa mja wengine na akaisisitiza juu yake, basi ni lazima atimize yote hayo na kuyakamilisha awezavyo. Na ndiyo maana Mwenyezi Mungu akakataza kuzivunja, akasema, "wala msivunje viapo baada ya kuvifunga imara" kwa kuvifunga kwa jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu, "Ilihali mmekwisha mfanya Mwenyezi Mungu" enyi mfungao mikataba "ndiye mdhamini wenu." Kwa hivyo si halali kwenu kutotekeleza yale mliyomfanya Mwenyezi Mungu kuwa ndiye mdhamini wenu, na hilo likawa ndani yake kuacha kumtukuza Mwenyezi Mungu na kumdharau. Na ilhali mwenzako aliridhia kiapo chako na uhakikisho ambao mlimfanya Mwenyezi Mungu kuwa ndiye mdhamini juu yake. Hivyo basi, kama alivyokuamini na akawa na dhana nzuri kwako, basi nawe mtimizie yale uliyosema na ukayasisitiza. "Hakika Mwenyezi Mungu anayajua myafanyayo," na atamlipa kila mtendaji kwa matendo yake kulingana na nia yake na makusudio yake.