انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · النحل
السورة ١٦

النحل

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٩

وَعَلَى ٱللَّهِ قَصْدُ ٱلسَّبِيلِ وَمِنْهَا جَآئِرٌ ۚ وَلَوْ شَآءَ لَهَدَىٰكُمْ أَجْمَعِينَ ٩

{9} Yeye Mtukufu alipotaja njia ya kihisia, na kwamba Mwenyezi Mungu amewafanyia waja kile wanachosafiri kwacho miongoni mwa ngamia na wengineo, akataja njia isiyo ya kihisia inayofikisha kwake. Akasema, "Na ni juu ya Mwenyezi Mungu kuelekeza Njia" ambayo ndiyo njia ya karibu zaidi na ya fupi zaidi, ifikishayo kwa Mwenyezi Mungu kwa utukufu wake. Na ama njia ya upotofu katika itikadi zake na matendo yake, ambayo ni kila njia inayopingana na njia yake iliyonyooka, basi hiyo inazuia kufika kwa Mwenyezi Mungu, na inafikisha katika nyumba ya taabu. Kwa hivyo wale walioongoka wakashika njia ile iliyonyooka kwa idhini ya Mola wao Mlezi, nao wapotovu wakapotea wakaiacha, na wakafuata njia za upotofu, "Na angelipenda, angeliwaongoa nyote." Lakini aliwaongoa baadhi kwa ukarimu wake na fadhila, na hakuwaongoa wengineo kwa hekima yake uadilifu wake.