النحل
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
ضَرَبَ ٱللَّهُ مَثَلًا عَبْدًا مَّمْلُوكًا لَّا يَقْدِرُ عَلَىٰ شَىْءٍ وَمَن رَّزَقْنَـٰهُ مِنَّا رِزْقًا حَسَنًا فَهُوَ يُنفِقُ مِنْهُ سِرًّا وَجَهْرًا ۖ هَلْ يَسْتَوُۥنَ ۚ ٱلْحَمْدُ لِلَّهِ ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ٧٥
{75} Mmoja wao ni mtumwa ambaye anamilikiwa, ambaye hajimiliki nafsi yake mwenyewe wala hamiliki chochote katika rasilimali za kidunia. Naye wa pili ni yule aliye huru, tajiri, ambaye Mwenyezi Mungu amemruzuku riziki nzuri ya kila aina ya mali, naye ni mkarimu apendaye kufanya hisani. Anatoa katika mali hiyo kwa siri na dhahiri. Je, huyu na yule ni sawa?! Hawako sawa, pamoja na kwamba wote ni viumbe ambao si muhali wao kuwa sawa. Kwa hivyo, ikiwa hawako sawa, basi vipi kiumbe - ambaye ni mja ambaye asiyemiliki chochote wala hana nguvu wala uwezo, bali ni mhitaji kwa namna zote - atakuwa sawa na Mola Mlezi, Muumba, Mmiliki wa falme zote, Muweza wa yote?! Ndiyo maana alijisifu yeye tu kwa aina zote za sifa njema, akasema, "Alhamdu Lillahi (Kuhimidiwa kote ni kwa Mwenyezi Mungu)!" Na ni kana kwamba ilisemwa: Kama ni hivyo, basi kwa nini washirikina waliwasawazisha miungu yao na Mwenyezi Mungu? Akasema, "Lakini wengi wao hawajui." Kwa maana, ikiwa wangejua elimu ya hakika, basi wasingethubutu kushirikisha huku kukubwa.