انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · النحل
السورة ١٦

النحل

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآيات ٦٣–٦٤

تَٱللَّهِ لَقَدْ أَرْسَلْنَآ إِلَىٰٓ أُمَمٍ مِّن قَبْلِكَ فَزَيَّنَ لَهُمُ ٱلشَّيْطَـٰنُ أَعْمَـٰلَهُمْ فَهُوَ وَلِيُّهُمُ ٱلْيَوْمَ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ٦٣ وَمَآ أَنزَلْنَا عَلَيْكَ ٱلْكِتَـٰبَ إِلَّا لِتُبَيِّنَ لَهُمُ ٱلَّذِى ٱخْتَلَفُوا۟ فِيهِ ۙ وَهُدًى وَرَحْمَةً لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ ٦٤

{63} Yeye Mtukufu alimbainishia Mtume wake - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - kwamba yeye si Mtume wa kwanza kukadhibiwa, akasema yeye Mtukufu, "Tallahi! Hakika tuliwatuma Mitume kwa umma zilizokuwa kabla yako" ili wawalinganie kumpwekesha Mwenyezi Mungu, "lakini Shetani akawapambia matendo yao;" kwa hivyo wakawakadhibisha Mitume hao, na wakadai kwamba hayo wanayofanya ndiyo haki inakayowaokoa kutokana na kila kichukizacho, na kwamba kile ambacho Mitume walilingania ni kinyume na hayo. Kwa hivyo, Shetani alipowapambia matendo yao, akawa yeye ndiye "kipenzi chao msaidizi" katika dunia, wakamtii, wakamfuata na wakamfanya kuwa kipenzi chao. "Je, mnafanya yeye na dhuria zake kuwa wapenzi wasaidizi wenu badala yangu, ilhali wao ni adui zenu? Ni mbaya mno badala hii ya madhalimu." "Nao wana adhabu chungu" Akhera, kwa maana waliacha kumfanya Mwingi wa rehema kuwa ndiye kipenzi msaidizi wao na wakaridhia kumfanya Shetani kuwa ndiye kipenzi msaidizi wao, kwa hivyo walistahili adhabu ya kudunisha kwa sababu ya hilo.