انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · النحل
السورة ١٦

النحل

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٦٠

لِلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِٱلْـَٔاخِرَةِ مَثَلُ ٱلسَّوْءِ ۖ وَلِلَّهِ ٱلْمَثَلُ ٱلْأَعْلَىٰ ۚ وَهُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلْحَكِيمُ ٦٠

{60} Na pindi huu ulipokuwa miongoni mwa mifano mibaya ambayo maadui zake washirikina walimnasibishia Mwenyezi Mungu, Yeye Mtukufu akasema, "Wale wasioiamini Akhera wana mfano mbaya mno." Yaani, mfano usio wenye mapungufu na kasoro kamili. "Naye Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye mfano bora zaidi" Nayo ni kila sifa ya ukamilifu. Kwa hivyo, kila ukamilifu uliopo, basi Mwenyezi Mungu anaustahiki zaidi bila hilo kuhitaji upungufu kwa namna yoyote ile. Naye anao mfano bora zaidi katika nyoyo za vipenzi wake, ambao ni kumpa taadhima, utukufu, upendo, kumrudia, na kumjua. "Naye ni Mwenye nguvu" ambaye alishinda vitu vyote, na viumbe vyote vilijisalimisha kwake. "Mwenye hekima" ambaye anaweka vitu mahali pake, kwa hivyo haamrishi wala kufanya chochote isipokuwa kile anachosifiwa juu yake kwa sababu ya ukamilifu katika hilo.