النحل
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَيَجْعَلُونَ لِمَا لَا يَعْلَمُونَ نَصِيبًا مِّمَّا رَزَقْنَـٰهُمْ ۗ تَٱللَّهِ لَتُسْـَٔلُنَّ عَمَّا كُنتُمْ تَفْتَرُونَ ٥٦
{56} Yeye Mtukufu anajulisha kuhusu ujinga wa washirikina na udhalimu wao na kumsingizia kwao uongo Mwenyezi Mungu , na kwamba wanaziwekea sanamu zao - ambazo hazijui wala hazinufaishi wala hazidhuru, - fungu katika kile ambacho Mwenyezi Mungu amewaruzuku na akawaneemesha kwayo. Kwa hivyo wakajisaidia na riziki yake katika kumshirikisha na wengine, na wakajikurubisha kwayo mbele ya masanamu yaliyochongwa, kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema, "Na walimwekea Mwenyezi Mungu fungu katika mimea na wanyama alioumba, wakasema: Hii ni sehemu ya Mwenyezi Mungu - kwa madai yao - na hii ni ya washirikishwa wetu. Basi vile vilivyokuwa vya washirikishwa wao, havimfikii Mwenyezi Mungu..." hadi mwisho wa Aya. "Tallahi! Bila ya shaka mtaulizwa kwa hayo mliyokuwa mnayazua!" Na mtaambiwa, "Je, Mwenyezi Mungu aliwaruhusu, au mnamzulia Mwenyezi Mungu tu?" Na nini dhana ya wale wanaomzulia uongo Mwenyezi Mungu Siku ya Qiyama? Basi atawaadhibu adhabu kali zaidi kwa hilo.