النحل
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَقَالَ ٱللَّهُ لَا تَتَّخِذُوٓا۟ إِلَـٰهَيْنِ ٱثْنَيْنِ ۖ إِنَّمَا هُوَ إِلَـٰهٌ وَٰحِدٌ ۖ فَإِيَّـٰىَ فَٱرْهَبُونِ ٥١
{51} Yeye Mtukufu anaamuru kwamba aabudiwe Yeye peke yake bila mshirika yeyote. Na hili linatumiwa kama ushahidi juu ya upekee wake katika kuneemesha [na Umoja]. Kwa hivyo, akasema, "Msijifanyie miungu wawili!" Yaani, msimfanyie mshirika yeyote katika uungu wake. Kwa maana yeye "Hakika ndiye Mungu Mmoja tu;" katika sifa zake zake kuu, ni wa kipekee katika vitendo vyote. Na kama vile Yeye ni Mmoja tu katika dhati yake, majina yake, sifa zake, na vitendo vyake, basi na mumfanyie yeye tu ibada. Na ndiyo maana akasema, "Basi niogopeni Mimi tu!" Yaani, nihofuni na mtekeleze amri yangu, na muepuke makatazo yao bila ya kunishirikisha na kiumbe chochote; kwani vyote hivyo vinamilikiwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu.