النحل
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
لِيُبَيِّنَ لَهُمُ ٱلَّذِى يَخْتَلِفُونَ فِيهِ وَلِيَعْلَمَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓا۟ أَنَّهُمْ كَانُوا۟ كَـٰذِبِينَ ٣٩ إِنَّمَا قَوْلُنَا لِشَىْءٍ إِذَآ أَرَدْنَـٰهُ أَن نَّقُولَ لَهُۥ كُن فَيَكُونُ ٤٠
{39 - 40} Kisha akataja hekima katika malipo na ufufuo, akasema, "Ili awabainishie yale waliyohitalifiana ndani yake" miongoni mwa masuala makubwa na madogo, kwa kubainisha uhakika wake na kuyaweka wazi. "Na ili wajue wale waliokufuru kwamba wao walikuwa waongo," [wakati] watayaona matendo yao watakuwa na majuto, na miungu wao ambao wanawaomba pamoja na Mwenyezi Mungu hawatawasaidia chochote wakati amri ya Mola wako Mlezi ilipokuja, na watakapoona kile wanachoabudu huku kikiwa kuni za Jahannam. Nalo jua na mwezi vitakunjwa, nazo nyota zitatawanyika, kisha itawawia wazi wale wanaoviabudu kwamba hivyo ni waja wa Mwenyezi Mungu waliotiishwa naye, na kwamba vinamhitaji Mwenyezi Mungu katika hali zote, na hayo siyo magumu wala mazito kwa Mwenyezi Mungu. Kwa maana, Yeye anapotaka kitu, anakiambia tu: kuwa, na linakuwa bila ya upinzani wala kukataa, bali linakuwa namna alivyotaka na kupenda.