النحل
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَقَالَ ٱلَّذِينَ أَشْرَكُوا۟ لَوْ شَآءَ ٱللَّهُ مَا عَبَدْنَا مِن دُونِهِۦ مِن شَىْءٍ نَّحْنُ وَلَآ ءَابَآؤُنَا وَلَا حَرَّمْنَا مِن دُونِهِۦ مِن شَىْءٍ ۚ كَذَٰلِكَ فَعَلَ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ فَهَلْ عَلَى ٱلرُّسُلِ إِلَّا ٱلْبَلَـٰغُ ٱلْمُبِينُ ٣٥
{35} Yaani, washirikina walitumia mapenzi ya Mwenyezi Mungu kuwa ndiyo ushahidi juu ya uhalali wa ushirikina wao, na kwamba Mwenyezi Mungu angelitaka, basi hawangemshirikisha na chochote wala hawangeliharimisha chochote katika wanyama hoa ambao amewahalalisha, kama vile Bahira, Wasila, Hami na mfano wa hao bila Yeye kusema hivyo. Na hii ni hoja batili. Kwa maana, ingekuwa ya kweli, basi Mwenyezi Mungu hangewaadhibu wale waliokuwa kabla yao pale walipomshirikisha, lakini aliwaadhibu adhabu kali sana. Na ikiwa alikuwa anayapenda hayo kwao, basi hangewaadhibu. Na makusudio yao katika hilo si isipokuwa kuikataa haki ambayo Mitume walikuja nayo. Vinginevyo, wanajua vyema kwamba hawana hoja yoyote dhidi ya Mwenyezi Mungu. Kwa maana, Mwenyezi Mungu aliwaamuru na kuwakataza, na akawawezesha kufanya kile alichowajukumisha, na akawapa nguvu na utashi ambao matendo yao yanatokana nao. Kwa hivyo kutumia kwao hukumu na majaliwa ya Mwenyezi Mungu kama ushahidi ni batili ya batili zote. Na kila mtu anajua vyema kihisia kwamba mwanadamu ana uwezo wa kufanya kila kitu anachotaka na hakuna yeyote anayepinga hilo. Na hawa walichanganya kati ya kumkadhibisha Mwenyezi Mungu, na kuwakadhibisha Mitume wake, na kukadhibisha mambo ya kiakili na kihisia. "Basi lipo lolote juu ya Mitume isipokuwa kufikisha tu kwa wazi" ambako kunafikia nyoyo na asibakie yeyote na hoja yoyote dhidi ya Mwenyezi Mungu. Na wakati Mitume wanawafikishia amri ya Mola wao Mlezi na katazo lake - nao wakayapinga haya kwa kutumia hukumu ya Mwenyezi Mungu na majaliwa kama ushahidi - basi Mitume hawana lolote katika jambo hilo, bali hesabu yao iko tu kwa Mwenyezi Mungu Mwenye Nguvu, Mtukufu.