النحل
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَقِيلَ لِلَّذِينَ ٱتَّقَوْا۟ مَاذَآ أَنزَلَ رَبُّكُمْ ۚ قَالُوا۟ خَيْرًا ۗ لِّلَّذِينَ أَحْسَنُوا۟ فِى هَـٰذِهِ ٱلدُّنْيَا حَسَنَةٌ ۚ وَلَدَارُ ٱلْـَٔاخِرَةِ خَيْرٌ ۚ وَلَنِعْمَ دَارُ ٱلْمُتَّقِينَ ٣٠
{30} Mwenyezi Mungu alipotaja kauli ya wale waliokadhibisha yale aliyoteremsha Mwenyezi Mungu, akataja yale waliyosema wachamungu, na walikubali na kukiri kwamba kile alichoteremsha Mwenyezi Mungu ni neema na heri kubwa ambayo Mwenyezi Mungu aliwaneemesha kwayo waja wake. Kwa hivyo wakakubali neema hiyo, na wakaipokea kwa kuikubali na kuifuata. Na wakamshukuru Mwenyezi Mungu kwa hilo, kwa hivyo wakaijua na kuifanyia kazi. "Kwa wale waliofanya mazuri" katika kumuabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu, na wakawafanyia uzuri waja wa Mwenyezi Mungu, basi hao wana "mazuri katika dunia hii" kama vile riziki pana, maisha mazuri, utulivu wa moyo, amani na furaha. "Na nyumba ya Akhera ni bora zaidi" kuliko nyumba hii na vyote vilivyomo miongoni mwa aina mbalimbali za starehe na matamanio. Kwani dunia hii, furaha yake ni kidogo ambayo imejaa masaibu na ni yenye kukatika, kinyume na starehe za Akhera. Na ndiyo maana akasema, "na ni njema mno nyumba hiyo ya wachamungu."