انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · النحل
السورة ١٦

النحل

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآيات ٢٦–٢٧

قَدْ مَكَرَ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ فَأَتَى ٱللَّهُ بُنْيَـٰنَهُم مِّنَ ٱلْقَوَاعِدِ فَخَرَّ عَلَيْهِمُ ٱلسَّقْفُ مِن فَوْقِهِمْ وَأَتَىٰهُمُ ٱلْعَذَابُ مِنْ حَيْثُ لَا يَشْعُرُونَ ٢٦ ثُمَّ يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ يُخْزِيهِمْ وَيَقُولُ أَيْنَ شُرَكَآءِىَ ٱلَّذِينَ كُنتُمْ تُشَـٰٓقُّونَ فِيهِمْ ۚ قَالَ ٱلَّذِينَ أُوتُوا۟ ٱلْعِلْمَ إِنَّ ٱلْخِزْىَ ٱلْيَوْمَ وَٱلسُّوٓءَ عَلَى ٱلْكَـٰفِرِينَ ٢٧

{26-27} "Walipanga njama wale waliokuwa kabla yao" dhidi ya Mitume wao, na wakafanya hila mbalimbali ili wakatae yale waliyowajia nayo, na wakajenga majumba makubwa kutoka kwa hila zao hizo. "Naye Mwenyezi Mungu akayasukua majengo yao kwenye misingi;" yaani, kikawa walichojenga hicho ni adhabu ambayo waliadhibiwa kwayo, "na adhabu ikawajia kutokea wasipohisi." Na hilo ni kuwa walidhani kwamba majengo hayo yatawanufaisha na kuwalinda kutokana na adhabu, lakini ikawa adhabu yao ni katika kile walichojenga na kukiwekea msingi imara. Na huu ni katika mifano mizuri zaidi katika kubatilisha kwa Mwenyezi Mungu njama za maadui zake. Kwa maana, walifikiria na kutathmini yale ambayo Mitume waliwajia nacho walipowakadhibisha, kisha wakawawekea misingi na kanuni batili ambazo wanazirudia na wanakataa kwazo yale waliyokuja nayo Mitume. Na pia wakafanya hila za kuwafikishia machukizo na madhara kwa Mitume na wale waliowafuata. Lakini njama zao hizo zikawa msiba juu yao, na kukawa kupanga kwao dhidi yao ni uharibifu juu yao wenyewe. Hayo ni kwa sababu njama zao hizo ni mbaya, na njama mbaya hazimsibu isipokuwa mwenyewe aliyezifanya. Hii ni katika dunia hii, nayo adhabu ya Akhera ni ya kuhizi zaidi, na ndiyo maana akasema, "Kisha Siku ya Qiyama atawahizi" mbele ya viumbe vyote na atawabainishia uongo wao na kumsingizia kwao Mwenyezi Mungu. "Na atasema, Wako wapi hao washirika wangu ambao kwao mlikuwa mkiwapinga (Manabii)?" Yaani, mliokuwa mkipigana na kumfanyia Mwenyezi Mungu uadui na kundi lake kwa ajili yao, huku mkidai kuwa wao ni washirika wa Mwenyezi Mungu. Na atakapowauliza swali hili, hawatakuwa na jibu isipokuwa kukiri upotovu wao na kukubali ukaidi wao, kwa hivyo watasema, "Wametupotea! Na watajishuhudia wenyewe kwamba walikuwa makafiri." "Watasema wale waliopewa elimu;" yaani, wanachuoni wamchao Mola wao Mlezi "Hakika hizaya leo;" yaani, Siku ya Qiyama. "Na ubaya;" yaani, adhabu "vitawashukia makafiri." Na katika hili kuna fadhila ya wenye elimu, na kwamba wao ndio wasemao ya haki katika dunia hii, na Siku watakaposimama mashahidi, na kwamba maneno yao yatazingatiwa na Mwenyezi Mungu na viumbe wake.