انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · النحل
السورة ١٦

النحل

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٢٤

وَإِذَا قِيلَ لَهُم مَّاذَآ أَنزَلَ رَبُّكُمْ ۙ قَالُوٓا۟ أَسَـٰطِيرُ ٱلْأَوَّلِينَ ٢٤

{24} Mwenyezi Mungu anasema kuwajulisha juu ya ukali wa kukadhibisha kwa washirikina ishara za Mwenyezi Mungu: "Na wanapoambiwa, "Ni nini alichoteremsha Mola wenu Mlezi?" Yaani, wanapoulizwa juu ya Qur-ani na Wahyi, ambao ndio neema kubwa zaidi ambayo Mwenyezi Mungu amewaneemesha waja, mnasemaje juu yake? Na je, mnashukuru neema hii na kuikiri, au mnaikufuru na kuifanyia ukaidi? Linakuwa jibu lao ni jibu baya na bovu zaidi. Wanasema juu yake: Ni "Hadithi za kubuni za wa mwanzo!" Yaani, uwongo ambao Muhammad alimzulia Mwenyezi Mungu, na ni hadithi tu za watu wa mwanzo ambazo watu hupitishana vizazi baada ya vizazi, ambazo baadhi yake ni ukweli na baadhi yake ni uwongo.