النحل
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
يُنَزِّلُ ٱلْمَلَـٰٓئِكَةَ بِٱلرُّوحِ مِنْ أَمْرِهِۦ عَلَىٰ مَن يَشَآءُ مِنْ عِبَادِهِۦٓ أَنْ أَنذِرُوٓا۟ أَنَّهُۥ لَآ إِلَـٰهَ إِلَّآ أَنَا۠ فَٱتَّقُونِ ٢
{2} Na alipojitakasa na yale waliyomuelezea nayo maadui zake, akataja ufunuo ambao anauteremsha juu ya manabii wake miongoni mwa yale yanayopasa kufuatwa katika kutaja yale yanayofailia kunasibishwa na Mwenyezi Mungu miongoni mwa sifa za ukamilifu. Kwa hivyo akasema, "Huwateremsha Malaika na ufunuo kwa amri yake juu ya amtakaye katika waja wake" katika wale anaowajua kwamba wanafailia hilo la kuubeba ujumbe wake. Na kiini cha wito wa wajumbe hao wote na pale inapozungukia miito hiyo ni kauli yake "kwamba onyeni kuwa hakuna mungu yeyote isipokuwa Mimi." Yaani, kumjua Mwenyezi Mungu, na kumpwekesha katika sifa za ukuu, ambazo ni sifa za uungu, na kumwabudu yeye peke yake bila ya mshirika yeyote. Kwani hilo ndilo aliloteremsha kwalo vitabu vyake, na akawatuma Mitume wake, na akafanya sheria zote kulingania hilo, na kuhimiza, na kupambana na mwenye kulipiga vita, na akafanya kinyume chake.