النحل
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
أَفَمَن يَخْلُقُ كَمَن لَّا يَخْلُقُ ۗ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ ١٧
{17} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja viumbe vikubwa alivyoviumba na neema za jumla alizoneemesha, akataja kwamba hakuna chochote kinachofanana naye, wala anayelingana naye wala mwenza. Akasema: "Ati yule anayeumba" viumbe vyote, naye hufanya atakavyo, "ni kama asiyeumba" chochote, si kidogo wala kingi? "Basi hebu hamkumbuki" mkajua kwamba aliye pekee katika uumbaji ana haki zaidi ya kuabudiwa kwa ibada zote? Kwa kuwa kama alivyo Mmoja katika uumbaji wake na uendeshaji wake, basi yeye ni Mmoja katika uungu wake, upweke wake, na kuabudiwa kwake. Na kama vile hakuwa na mshirika yeyote alipowaumba na akaumba wasiokuwa nyinyi, basi msimfanyie wenza katika ibada yake, bali mpwekesheeni Dini.